Pages

Monday, March 17, 2014

Wanajeshi wa Uganda kuondoka Sudan Kusini

Uganda imesema itaondoa wanajeshi wake walioko nchini Sudan Kusini baada ya kikosi kinachoundwa na nchi za Afrika Mashariki kupelekwa nchini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Jinja, Mkuu wa jeshi la Uganda Jenerali  Katumba Wamala amesema kuondoka kwao nchini Sudan Kusini kunategemea kuwasili kwa kikosi hicho cha pamoja cha nchi za Afrika Mashariki. Ikumbukwe kuwa kikao cha dharura cha viongozi wa Jumuiya ya kieneo ya nchi za mashariki mwa Afrika IGAD kilifanyika Alkhamisi nchini Ethiopia kujadili kadhia ya Sudan Kusini. Viongozi wa IGAD waliafiki kutuma askari wa kulinda amani katika nchi hiyo iliyotumbukia katika vita vya ndani kuanzia Desemaba mwaka jana. Wakati huo huo waasi wa Sudan Kusini wamepinga pendekezo la kutumwa askari wa Afrika Mashariki nchini humo. Msemaji wa waasi Taban Deng amedai kuwa IGAD inaipendelea serikali ya Rais Salva Kiir katika mgogoro wa Sudan Kusini.

Imearifiwa karibu watu elfu 10 wameuawa katika mapigano ambayo yamechukua muelekeo wa kikabila kati ya kabila la Nuer la kiongozi wa waasi na makamu wa rais wa zamani Riek Machar na kabila la Dinka la Rais Kiir

No comments:

Post a Comment