Pages

Friday, March 14, 2014


Ban Ki moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amekutana na viongozi wa kidini wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na kusisitiza juu ya wajibu wa kutumwa askari zaidi wa kusimamia usalama na amani nchini humo. Katika kikao hicho, Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, amewasifu viongozi hayo wa dini mbalimbali nchini humo na kuwataja kuwa ni nembo ya kuishi pamoja kwa amani na ni moja ya nguzo muhimu za jamii ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Ameongeza kuwa, kwa bahati mbaya kabisa nembo hiyo inakabiliwa na tishio kubwa la kusambaratika. Kwa upande mwingine, Ban Ki moon amewataka viongozi hao wa kidini, kufanya juhudi za kina za kuzuia kile alichosema kuwa ni mpasuko na mgawanyiko wa kijamii nchini humo. Kwa upande wao Askofu Dieudonné Nzapalainga na Sheikh Oumar Kobine Layama, wameelezea kusikitishwa na hali mbaya ilivyo nchini mwao na kuitaka jamii ya kimataifa kusaidia kumaliza machafuko na mauaji hasa yanayofanywana Wakristo dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo. Askofu Nzapalainga pia amepinga kuwepo uadui kati ya jamii za Waislamu na Wakristo nchini humo na amewakana waasi wa Kikristo wa Anti Balaka akisema hawaiwakilishi dini hiyo kwa vitendo vyao hivyo vya kikatili.

No comments:

Post a Comment