Friday, March 14, 2014
Rais wa TZ kumwapisha Katibu wa Bunge la Katiba
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, leo asubuhi anatazamiwa kumwapisha Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Bwana Yahya Khamis Hamad, kuwa Katibu wa Bunge Maalum la Katiba nchini humo. Aidha katika sherehe fupi itakayofanyika Ikulu Ndogo mjini Dodoma, Rais Kikwete atamwapisha Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Thomas Didimu Kashililah kuwa Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba la nchi hiyo.
Viongozi hao yaani Bw. Hamad na Dkt. Kashilillah wanashika nafasi hizo kwa mujibu wa Kifungu cha 24 (1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Tanzania. Kwa mujibu wa kifungu cha 24 (3) cha sheria hiyo, Katibu wa Bunge Maalumu anatakiwa kutoka upande tofauti na ule anakotoka Mwenyekiti wa Bunge hilo. Kwa ajili hiyo, na kwa kuzingatia kuwa, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba Tanzania, Bwana Samuel John Sitta ametoka Tanzania Bara, Katibu wa Bunge hilo Bwana Yahya Khamis Hamad na ambaye ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi anatoka upande wa pili wa Muungano, yaani Zanzibar.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment