Pages

Thursday, March 13, 2014

Niger: Hatukuchukua hongo juu ya mwana wa Gaddaf


Niger: Hatukuchukua hongo juu ya mwana wa GaddafiWaziri wa Vyombo vya Mahakama nchini Niger, amekadhibisha tuhuma kwamba, nchi yake ilihongwa dola milioni 20 za Kimarekani na serikali ya Libya, kwa ajili ya kumkabidhi mwana wa Kanali Muammar Gaddafi kwa serikali ya Tripoli. Marou Amadou, Waziri wa Vyombo vya Mahakama na Msemaji wa Serikali ya Niger, ameelezea kusikitishwa kwake na kusambazwa habari hizo zisizo na ukweli wowote na kuongeza kuwa, katika kumkabidhi Saadi el-Qaddafi kwa serikali ya Tripoli, nchi yake haikupokea hongo yoyote. Vile vile amesema, Niger haikupokea hongo yoyote pia katika kumkabidhi Abdallah Mansour aliyekuwa kamanda wa ngazi za juu katika utawala uliopita wa Libya. Amewataka waandishi wa habari kuzifanyia utafiti habari kabla ya kuziandika. Saadi el-Qaddafi (40), anakabiliwa na tuhuma za kuhusika na jinai mbalimbali wakati wa kujaribu kuubakisha madarakani utawala wa baba yake katika machafuko ya mwaka 2011 nchini Libya. Mwezi Disemba mwaka 2011 muda mchache kabla ya kuanguka utawala wa Kanali Muammar Gaddafi, Saadi el-Qaddafi, aliomba hifadhi katika nchi jirani ya Niger.

No comments:

Post a Comment