Friday, March 14, 2014
Guterres: Waislamu watamalizwa CAR
Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwashughulikia wakimbizi UNHCR, Antonio Guterres ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba, hatua za haraka zisipochukuliwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Waislamu wa nchi hiyo watauawa wote.
Mkuu huyo wa UNHCR ameongeza kuwa, kundi la Kikristo la Anti-Balaka limehamia magharibi mwa CAR wanakoishi Waislamu wengi na kwamba yumkini wakafanya mauaji ya kutisha dhidi ya Waislamu hao.
Hii ni katika hali ambayo, Waziri wa Mambo ya Nje wa serikali ya mpito ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, Toussaint Kongo-Doudou, ameliomba Baraza la Usalama la UN liidhinishe kupelekwa wanajeshi zaidi nchini humo ili kudhibiti hali ya mambo. Kongo-Doudou amesema mauaji dhidi ya Waislamu yakiendelea itafika mahali nchi itasambaratika na itakuwa vigumu kudhibiti hali ya mambo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment