Monday, March 17, 2014
Kuanza vita vya kiuchumi baina ya Marekani na China
Gazeti la The Hill linalochapishwa nchini Marekani limeandika habari za kuanza vita vya kiuchumi baina ya nchi hiyo na China. Gazeti hilo limeandika kuwa, Washington inapanga mikakati ya kutiliana saini na nchi za Umoja wa Ulaya na zile zilizopo pambizoni mwa bahari ya Pasifiki ya kuzuia nguvu za kiuchumi za China. Msemaji wa Ofisi ya mwakilishi wa Marekani katika Shirika la Biashara Duniani ameliambia gazeti hilo kwamba makubaliano hayo ya pamoja kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya ni hatua ya pamoja ya kukabiliana na wahka uliokuwa nazo nchi hizo kuhusiana na masuala ya biashara ulimwenguni. Imeelezwa kuwa, Marekani imeamua kuchukua uamuzi huo kwa hofu kwamba nguvu na satua zake za kiuchumi zinazopungua siku hadi siku zitachukuliwa na China. Wakati huohuo, China nayo imeeleza kuwa, mikakati ya Marekani ya kuleta mabadiliko kwenye sheria za ndani nchini humo, imegonga mwamba. Hii ni katika hali ambayo, Kongresi na Ikulu ya Marekani kwa pamoja zinafanya juhudi za kufanya miamala mikubwa ya kiuchumi ambayo inahofiwa kuzusha vita vya kiuchumi kati ya nchi hiyo na China katika miaka ijayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment