Pages

Friday, March 14, 2014

Serikali ya Mauritania yapinga watakavyo wapinzani




Serikali ya Mauritania imepinga pendekezo la wapinzani wa nchi hiyo, la kutaka kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa rais. Waziri wa Mawasiliano na mahusiano ya bunge na msemaji wa serikali ya Mauritania, Sidi Mohamed Ould ameyasema hayo baada ya kumalizika kikao cha baraza la mawaziri wa nchi hiyo, na kuongeza kuwa, serikali haitaunda serikali ya umoja wa kitaifa kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu na kwamba pendekezo hilo la wapinzani halikubaliki kabisa. Sidi Mohamed amesisitiza juu ya kwamba, uchaguzi mkuu nchini Mauritania, utafanyika katika tarehe iliyopangwa na kwamba hakutafanyika ucheleweshaji wowote. Aidha amesisitiza kuwa, serikali ya Nouakchott imejiandaa kufanya mazungumzo na makundi na mirengo yote ya kisiasa nchini humo. uchaguzi mkuu nchini Mauritania umepangwa kufanyika mwaka huu wa 2014, hata hivyo haijatangazwa tarehe rasmi ya kufanyika uchaguzi huo. Inaelezwa kuwa Rais Mohamed Ould Abdel Aziz wa nchi hiyo, atashiriki katika king'anyiro hicho.

No comments:

Post a Comment