Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai amekadhibisha kuwepo hatari ya kusambaratika chama chake cha Movement for Democratic Change MDC. Tsvangirai aliyasema hayo jana na kuongeza kuwa, chama chake kiko hai na kitaendelea kubakia hivyo na kwamba, hakuna hatari yoyote ya kukisambaratisha. Ameongeza kuwa, anaendelea kufanya juhudi za kuimarisha umoja ndani ya chama hicho. Hata hivyo Morgan Tsvangirai amekiri kuwepo kwa matatizo ndani ya chama cha MDC lakini akasisitiza kuwa, matatizo hayo yatatatuliwa haraka iwezekanavyo. Hii ni katika hali ambayo naibu wa Muweka Hazina Mkuu wa chama hicho Bwana Stanley Manguma amekuwa akimtaka Tsvangirai ajiuzulu nyadhifa zake chamani kutokana na kushindwa na Rais Robert Mugabe katika uchaguzi mkuu uliopita. Kabla ya hapo kulivuma habari kuwa wafuasi wa Tsvangirai walimshambulia Manguma akiwa katika ofisi za chama hicho jijini Harare.
Friday, March 14, 2014
Tsvangirai: Chama cha MDC kitaendelea kuwa imara

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment