Friday, March 14, 2014
Viongozi wa serikali Kenya kupunguziwa mishahara
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametangaza kuwa, yeye na Naibu wake William Ruto wameridhia mishahara yao ipunguzwe kwa asilimia 20 ili kupunguza matumizi ya serikali.
Rais Kenyatta pia amesema mawaziri wote 18 na makatibu wakuu wa wizara wameridhia mishahara yao ipunguzwe kwa asilimia 10 ili kufanikisha lengo hilo. Rais Kenyatta na Naibu wake wamekuwa wakikutana na mawaziri wao kwa siku tatu mfululizo kwenye kongamano lililojadili utendaji wa serikali ndani ya muda wa mwaka mmoja uliopita. Rais wa Kenya amesema serikali yake itabuni sheria mpya inayohusiana na safari za nje ya nchi ambapo maafisa wa serikali wataruhusiwa kusafiri nje iwapo tu patakuwa na ulazima wa kufanya hivyo.
Matumizi ya serikali hayapaswi kuvuka asilimia 7 ya mapato ya nchi kwa mwaka lakini nchini Kenya, matumizi hayo yamekuwa yakipanda na kufikia asilimia 12 katika bajeti ya mwaka 2013-2014.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment