Pages

Friday, March 14, 2014

Ijumaa, Machi 14, 2014 katka historia




Leo ni Ijumaa tarehe 12 Mfunguo Nane Jamadil Awwal 1435 Hijria sawa na 14 Machi mwaka 2014.

 

Siku kama ya leo miaka 36 iliyopita jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel lilianza kuivamia na kuikalia kwa mabavu ardhi ya Lebanon kwa kisingizio cha kukabiliana na operesheni iliyofanywa na wanamapambano wa Kipalestina pambizoni mwa Tel Aviv. Katika mashambulio hayo jeshi la Israel liliua raia wengi wasio na hatia wa Lebanon na Palestina na kukalia kwa mabavu sehemu ya ardhi ya Lebanon. Hata hivyo utawala huo ghasibu uliondoka kwa fedheha katika maeneo ya kusini mwa Lebanon mwaka 2000 baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa wanamapambano wa Hizbullah na kuondoka kwenye eneo hilo.

Siku kama ya leo miaka 135 iliyopita, inayosadifiana na tarehe 14 Machi 1879 alizaliwa Albert Einstein, msomi mashuhuri wa fizikia na hisabati nchini Ujerumani. Mnamo mwaka 1921 msomi huyo alipewa tuzo ya Nobel katika taaluma ya fizikia, baada ya kufanya juhudi kubwa za kiutafiti. Utafiti na nadharia za Einstein katika uwanja wa nyuklia zilikuwa na taathira kubwa duniani. Hata hivyo Einstein alisikitika sana baada ya kugundua kwamba uchunguzi na utafiti wake katika uwanja wa atomu umetumiwa na baadhi ya nchi kwa ajili ya kutengeneza silaha hatari za nyuklia. Albert Einstein alifariki dunia 1955.

Na siku kama hii ya leo miaka 482 iliyopita alifariki dunia msomi mkubwa wa Kiislamu Ibn Tulun Dimashqi, aliyekuwa faqihi, mwanafasihi na mwanahistoria. Ibn Tulun katika umri wake wote alifanya jitihada kubwa za utafiti, kufundisha na kuandika vitabu vya taaluma mbalimbali. Ibn Tulun Dimashqi ameandika vitabu vingi vya thamani kuhusiana na historia ya Kiislamu na pia katika uwanja wa tafsiri ya Qur'ani Tukufu, hadithi, lugha, tiba na irfani.

No comments:

Post a Comment