Friday, March 14, 2014
Rais wa zamani wa Sierra Leone afariki dunia
Rais wa zamani wa Sierra Leone, Ahmad Tejan Kabbah amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82. Habari iliyotolewa na ikulu ya rais ya nchi hiyo, imetangaza kufariki dunia rais huyo wa zamani wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika na kumtaja kwamba aliyekuwa mtu muhimu kwa taifa hilo. Mbali na Ikulu ya Rais ya Sierra Leone kutoa salamu za rambirambi kwa familia na kwa taifa zima kwa msiba huo, pia imetangaza siku saba za maombolezo kuanzia leo na bendera kupeperushwa nusu mlingoti. Vyombo mbalimbali vya ndani ya Sierra Leone, vimeinukuu familia ya hayati Ahmad Tejan Kabbah, ikisema kuwa, amefariki dunia akiwa nyumbani kwake Freetown, mji mkuu wa Sierra Leone na karibu na mke na familia yake. Miezi michache iliyopita, Ahmad Tejan Kabbah alipelekwa mjini London, Uingereza kwa ajili ya matibabu. Aliongoza nchi hiyo kwa mihula miwili na kumuachia madaraka Rais wa sasa Ernest Bai Koroma mwaka 2007.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment