Pages

Monday, March 17, 2014

Iran yanyakua ubingwa wa dunia wa mieleka


 

Timu ya taifa ya mchezo wa mieleka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeunyakua ubingwa wa dunia kwenye mtindo wa freestyle, baada ya kuibwaga Russia kwa ushindi wa 6 kwa 2, kwenye mchezo wa fainali uliofanyika mapema leo asubuhi  huko Los Angeles nchini Marekani. Timu ya mieleka ya Iran imefanikiwa kutetea taji hilo, baada ya kuibwaga India katika mchezo wa nusu fainali. Kabla ya hapo, timu ya mieleka ya Iran ilifanikiwa kuisambaratisha Armenia, Uturuki, wenyeji Marekani, India na hatimaye Russia katika mechi ya fainali. Kwenye mashindano hayo, wenyeji  Marekani  imeshika nafasi ya tatu baada ya kuibwaga  Ukraine.

No comments:

Post a Comment