Pages

Monday, March 17, 2014

Marekani iko tayari kuiwekea vikwazo zaidi Russia


 

Rais Barack Obama wa Marekani amemtahadharisha mwenzake Vladmir Putin wa Russia kwamba Washington na waitifaki wenzake wa Ulaya kamwe hawatayatambua rasmi matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika katika kisiwa cha Crimea nchini Ukraine. Rais Obama ameongeza kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa kuwekwa vikwazo vipya dhidi ya Russia na kusisitiza kwamba Washington na jamii ya kimataifa hazitayatambua matokeo ya kura hiyo ya maoni kwani inakiuka wazi katiba ya Ukraine. Kwa upande mwingine, Rais Putin amesema kuwa, ni suala la kimantiki la  kufanyika kura ya maoni katika kisiwa hicho. Mkuu wa Kamisheni ya Uchaguzi ya Crimea amesema kuwa asilimia 95.5 ya wananchi waliopiga kura hiyo wanataka kisiwa hicho kiungane na Russia. Taarifa ya kamisheni hiyo inaeleza kuwa, zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa kisiwa cha Crimea walishiriki kwenye zoezi hilo la kura ya maoni la kuainisha mustkabili wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment