Pages

Thursday, March 13, 2014

LEO KATIKA HISTORIA

Alkhamisi, Machi 13, 2014
Leo ni Alkhamisi tarehe 11 Mfunguo Nane Jamadil Awwal 1435 Hijria sawa na Machi 13, 2014.
Siku kama ya leo miaka 31 iliyopita, inayosadifiana na 13 Machi 1983, Joshua Nkomo kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe alikimbilia nchini Uingereza akihofia usalama wa maisha yake. Nkomo ambaye alikiongoza chama cha Zimbabwe African People's Union (ZAPU) alisema kuwa, alilazimika kutoroka nchini Zimbabwe na kukimbilia Uingereza kwa kuwa maisha yake yalikuwa hatarini. Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya Brigedi ya Tano ya jeshi la Zimbabwe kuizingira kambi yake iliyoko katika mji wa Bulawayo.
Tarehe 13 Machi miaka 66 iliyopita Wazayuni waliokuwa na mfungamano na kundi la kigaidi la Haganah, walishambulia kitongoji cha Wapalestina cha Husseiniyah katika eneo la kaskazini mwa Jalilah. Wazayuni hao waliua shahidi zaidi ya Wapalestina 60 na kuharibu nyumba zao kadhaa. Katika siku hiyohiyo, wanajeshi wa Israel walizilipua kwa mabomu nyumba za Wapalestina katika eneo la 'Qatmuun' lililoko Baitul Muqaddas. Mauaji ya Waislamu wa Palestina yaliyofanywa na makundi ya kigaidi ya Israel, yalitekelezwa kwa lengo la kutaka kutangaza uwepo wa utawala huo bandia kwenye ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina baada ya kuondoka vikosi vya majeshi ya Uingereza katika eneo hilo.
Na siku kama ya leo miaka 281 iliyopita, inayosadifiana na 13 Machi, 1733 alizaliwa Joseph Priestley, mkemia na mwanafizikia wa Uingereza. Priestley alikuwa mashuhuri mno hasa katika taaluma ya kemia. Katika uchunguzi na utafiti wake, aliweza kuvumbua uvutaji pumzi katika mimea na hewa za oksijeni na nitrogen. Joseph Priestley alifariki dunia mwaka 1804.

No comments:

Post a Comment