Pages

Friday, March 14, 2014

Hatima ya ndege ya abiria ya Malaysia yatatanisha





Ndege ya abiria ya shirika la ndege la Malaysia iliyokuwa na abiria 227 na wahudumu 12 imetoweka ikiwa katika anga ya bahari ya kusini mwa China na kuhofiwa kuwa imeanguka. Shirika la ndege la Malaysia limetangaza leo kuwa timu za utafutaji na uokoaji zimetumwa katika maeneo ya baharini ambayo huenda ndege hiyo itakuwa imeangukia. Endapo kuanguka kwa ndege hiyo aina ya Boeing 777- 200ER kutathibitishwa, hiyo itakuwa ajali ya maafa makubwa zaidi kwa ndege za aina hiyo zilizotengenezwa nchini Marekani tangu zilipoanza kutoa huduma za usafiri wa anga miaka 19 iliyopita. Taarifa za vyombo vya habari zinaeleza kuwa zaidi ya ndege 12 na meli zipatazo tisa zinaendesha operesheni ya kuitafuta ndege hiyo iliyopoteza mawasiliano masaa mawili baada ya kuondoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuala Lumpur Malaysia ikitarajiwa kuwasili mji mkuu wa China, Beijing asubuhi ya leo. Kwa mujibu wa shirika la habari la China Xinhua, mawasiliano yalipotea wakati ndege hiyo ilipokuwa ikikaribia anga ya Vietnam. Imeelezwa kuwa miongoni mwa abiria 227 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo, 153 ni raia wa China au Taiwan, 38 kutoka Malaysia, Waindonesia saba, raia watano wa India na Waustralia sita…/

No comments:

Post a Comment