Pages

Saturday, March 15, 2014

Vijana J/Afrika ya Kati waunda makundi ya kujilinda




Hii ndiyo hali ya Waislamu Jamhuri ya Afrika ya Kati

Vijana wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, wameunda makundi ya kujitolea kwa lengo la kujilinda nchini humo. Makundi hayo yanayoundwa na kati ya watu watano hadi 10 na yasiyo na silaha, yatakuwa na jukumu la kuwalinda Waislamu kutokana na mashambulizi ya waasi wa Kikristo wa Anti-Balaka. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, lengo la makundi hayo ni kuzuia mauaji na uporaji wa mali za raia wa mji wa Bangui, wakiwemo Waislamu. Aidha makundi hayo ya kujilinda yametoa onyo kali kwa waasi hao wa Kikristo wa Anti-Balaka kutokana na ukatili wao dhidi ya Waislamu. Habari zaidi zinasema kuwa, makundi hayo yataenea katika maeneo tofauti ikiwamo mabarabarani mjini Bangui. Hatua hiyo imekuja baada ya vikosi vya kigeni vikiwemo vile vya Ufaransa, kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kurejesha usalama nchini humo, huku mauaji dhidi ya Waislamu yakiendelea siku hadi siku.

No comments:

Post a Comment