Pages

Monday, March 17, 2014

Video inayoonesha gaidi wa Syria akikiri kuvunja misikiti ya Ahlu Sunna


 

Ingia chini ya habari hii kuona video inayomuonesha kijana wa Kitunisia ambaye hivi karibuni amerejea nchini Tunisia  akitokea Syria ambako alikuwa akipambana bega kwa bega na makundi ya kigaidi nchini humo.

Kijana huyo amesema kuwa moja ya majukumu yao nchini Syria lilikuwa ni kubomoa Misikiti ya Waislamu wa Madhehebu ya Ahlul Sunna na hasa misikiti iliyokuwa na majina ya makhalifa au Bibi Aysha, na kisha kulitupia lawama jeshi la Syria ya kuharibu misikiti hiyo.

Abu Qusway ameongeza kuwa, mkakati huo ulifanyika kwa shabaha ya kuwakasirisha wanajeshi hao ambao wengi wao ni Masuni ili wajitenge na serikali ya Syria. Ameongeza kuwa, wanawake waliopelekwa Syria kutoka nchi za Kaskazini mwa Afrika walikuwa na jukumu la kuwapiga risasi wanajeshi na raia kwa kuvizia.

Kijana huyo wa Tunisia ameiambia Televisheni ya al Mayadin kuwa, alichukua maamuzi ya kuwauwa wapiganaji wenzake ili aweze kurejea nchini Tunisia kwa uhuru kamili, kinyume cha hivyo asingeliweza kuruhusiwa kurudi. Kijana huyo amesema kuwa, nchi za Qatar, Saudi Arabia Uturuki na nchi nyingine za Magharibi zimekuwa zikitoa misaada ya kisilaha, kifedha na kilojistiki kwa makundi ya kigaidi nchini Syria.bonyeza hapa kuangaia.>>http://kiswahili.irib.ir/habari/mchanganyiko/item/38880-video-inayoonesha-gaidi-wa-syria-akikiri-kuvunja-misikiti-ya-ahlu-sunna

Marekani iko tayari kuiwekea vikwazo zaidi Russia


 

Rais Barack Obama wa Marekani amemtahadharisha mwenzake Vladmir Putin wa Russia kwamba Washington na waitifaki wenzake wa Ulaya kamwe hawatayatambua rasmi matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika katika kisiwa cha Crimea nchini Ukraine. Rais Obama ameongeza kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa kuwekwa vikwazo vipya dhidi ya Russia na kusisitiza kwamba Washington na jamii ya kimataifa hazitayatambua matokeo ya kura hiyo ya maoni kwani inakiuka wazi katiba ya Ukraine. Kwa upande mwingine, Rais Putin amesema kuwa, ni suala la kimantiki la  kufanyika kura ya maoni katika kisiwa hicho. Mkuu wa Kamisheni ya Uchaguzi ya Crimea amesema kuwa asilimia 95.5 ya wananchi waliopiga kura hiyo wanataka kisiwa hicho kiungane na Russia. Taarifa ya kamisheni hiyo inaeleza kuwa, zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wa kisiwa cha Crimea walishiriki kwenye zoezi hilo la kura ya maoni la kuainisha mustkabili wa eneo hilo.